Kesi ya kiongozi wa upinzani Tanzania yaahirishwa

  • | Citizen TV
    1,016 views

    Haya yakijiri nchini, kesi ya uhaini dhidi ya kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu imeahirishwa hadi tarehe 16 mwezi juni. Akiongoza kesi hii, Hakimu mkuu Godfrey Mhini ameagiza upande wa mashtaka kuwasilisha hali ya uchunguzi na endapo wananuiya kumfungulia mashtaka kiongozi huyo wa Chadena kufuatia kukaa kwake korokoroni kwa takriban miezi miwili. Kwenye kesi hii dhidi ya Tundu Lissu, mahakama pia imemtaka kiongozi huyu wa upinzani na wafuasi wake kuheshimu mahakama.