Polisi wawazuilia washukiwa 7 kwa madai ya mauaji

  • | Citizen TV
    2,851 views

    Maafisa wa usalama kaunti ya Nakuru wanawazuiliwa washukiwa saba kuhusiana na mauaji ya afisa wa polisi na kujeruhiwa kwa wengine wawili. Afisa huyo wa kituo cha polisi cha Bondeni, aliuawa kwa kupigwa risasi baada ya kushambuliwa na genge la wahalifu jumapili usiku. Polisi wanasema wamenasa bunduki kutoka kwa washukiwa wanaozuiliwa.