Mpango wa majaribio wa chakula shuleni waanzishwa katika kaunti kame

  • | KBC Video
    32 views

    Tatizo la kuacha shule na kutohudhuria masomo miongoni mwa wanafunzi limekuwa suala la kuibua wasiwasi katika maeneo kame kutokana na ukame wa muda mrefu. Njaa miongoni mwa wanafunzi inasababisha kutatizika kwa masomo na inaathiri matokeo ya mitihani yao katika maeneo hayo. Ili kukabiliana na changamoto hii, shirika la kushughulikia maslahi ya watoto humu nchini, chini ya idara mpya ya serikali ya kushughulikia maslahi ya watoto, limeanzisha mpango wa majaribio wa lishe shuleni katika kaunti za maeneo hayo ili kukabiliana na uhaba wa chakula.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive