Waislamu kote ulimwenguni wameadhimisha siku ya Arafah

  • | Citizen TV
    1,087 views

    Waislamu kote ulimwenguni wameadhimisha siku ya Arafah ambayo ni siku ya 9 ya mwezi wa mwisho katika kalenda ya Kiislamu. Ni siku ambayo ina umuhimu mkubwa kwa jamii ya Waislamu huku pia ikiwa siku muhimu zaidi ya ibada ya Hajj ambako waisilamu kote duniani husafiri kwenda kwa ibada hii mjini Makkah nchinI Saudi Arabia.