Kazi Mtaani I Vijana waanza kujisajili kwa mpango wa Climate Worx

  • | KBC Video
    44 views

    Serikali imetangaza kurejelewa kwa mpango wa Kazi Mtaani chini ya jina jipya, Climate Worx unaotarajiwa kung’oa nanga mwezi Julai mwaka huu. Katibu katika idara ya nyumba Charles Hinga amesema jumla ya vijana elfu-113 kutoka kaunti zote 47 watashirikishwa katika mradi huo. Vijana wanaotumainia kuajiriwa katika mpango huo wamehimizwa wajisajili mtandaoni kupitia tovuti ya www.crsp.co.ke. Jumla ya shilingi bilioni-5 kutoka wizara ya barabara zimetengwa kufanikisha mradi huo kwa muda wa miezi sita. Tangazo hilo linajiri baada ya rais William Ruto kusema mradi huo utazinduliwa kote nchini hivi karibuni.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive