Wakazi wa Angata Barikoi waandamana kutokana na mizozo ya ardhi Narok

  • | Citizen TV
    1,265 views

    Watu kadhaa wanaendelea kuuguza majeraha katika hospitali ya Narok Kusini , kutokana na mzozo wa kipande cha ardhi cha ekari 110. Makundi mawili yanadai umiliki wa shamba hilo, hali ambayo imesababisha vita. Huku hayo yakijiri, wakazi wa Angata Barrikoi kaunti hiyo hiyo waliandamana wakilalamikia mashambulizi ya mara kwa mara katika eneo hilo.