Waislamu kote nchini waadhimisha sherehe za Eid-ul-Adha

  • | KBC Video
    22 views

    Waumini wa Kiislamu walikusanyika kwenye maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya swala za Eid-ul-Adha, kuashiria mwanzo wa siku tatu za kilele cha sherehe hizi. Waumini walikusanyika kwenye sehemu wazi kuswali kabla ya karamu na tafrija ambazo kwa desturi hufanyika siku hii. Miito ya kudumisha umoja na kuwakumbuka maskini katika jamii ilisheheni. Eid-ul-Adha inasadifiana na hija ya kila mwaka ya mji Mtakatifu wa Mecca inayofanyika mwezi wa Dhu-al-Hijjah, ambao ni mwezi wa mwisho katika kalenda ya Kiislamu.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive