Viongozi wa upinzani wakosoa mpango wa kuchangisha pesa

  • | Citizen TV
    1,078 views

    Viongozi wa upinzani sasa wameikashifu miradi ya uchangishaji fedha inayoendelea, wakisema ni ishara ya utepetevu wa serikali. Wakizungumza katika sehemu mbali mbali, viongozi hao wamesema kuwa sharti serikali iwajibike katika kubuni sera za kulikwamua taifa kutoka lindi la ukosefu wa ajira na gharama ya juu ya maisha. Aidha wamesema kuwa watahakikisha kuwa wanamuondoa uongozini rais William Ruto katika uchaguzi mkuu ujao, wakidai ameshindwa kutimiza ahadi alizotoa kwa wakenya.