Kikundi cha kutathmini kisukari kimeandaa michezo

  • | Citizen TV
    82 views

    Kikundi cha kutathmini ugonjwa wa kisukari kimeandaa siku yake ya michezo kwa mara ya kwanza kikileta pamoja madaktari na jamii katika uwanja wa huduma za jamii hapa nairobi. Wakati wa michezo hiyo, jamii imetakiwa kujitokeza kupimwa kisukari ili kuepuka idadi kubwa inayozidi kunakiliwa ya wagonjwa wa maradhi hayo. Michezo kama soka, riadha, voliboli na ulengaji shabaha ilishirikishwa kwenye mashindano hayo.