Albert alifanywaje seli?

  • | Citizen TV
    5,332 views

    Imebainika kuwa mwanablogu Albert Ojwang alifariki saa moja baada ya kufikishwa katika kituo cha polisi cha Central. Haya yamebainika kwenye jedwali la polisi katika kituo cha central huku uchunguzi kuhusu kifo cha ojwang mikononi mwa polisi ukiendelea. Ripoti ndani ya kituo hizo zikibainisha kuwa, damu nyingi ilimwangika muda huo ambapo ojwang alikuwa amezuiliwa. Mwanahabari wetu ode francis anatuletea picha za pekee za ndani ya seli alikokuwa amezuiliwa marehemu mwanablogu huyo.