Shilingi Bilioni 246.24 zitatumiwa kulipa madeni ya nje

  • | Citizen TV
    687 views

    Serikali italazimika kukopa zaidi na kutumia zaidi ya shilingi trilioni moja kulipa madeni. Kwenye makadirio ya bajeti mwaka huu, waziri wa hazina ya kitaifa John Mbadi ametenga shilingi trilioni 1.09 kulipia madeni ambapo ni ongezeko la shilingi bilioni 94.2 zilizotumiwa mwaka wa kifedha wa 2024/2025. Haya ni huku shilingi bilioni 851.4 ya pesa hizo ikitumiwa kulipa madeni ya humu nchini na shilingi bilioni 246.24 zikitumiwa kulipa madeni ya nje.