Bajeti ya kwanza ya Waziri John Mbadi huku alifuata desturi ya kutembea na mkoba

  • | Citizen TV
    4,368 views

    Imekuwa bajeti ya kwanza ya Waziri wa hazina ya kitaifa John Mbadi. Na kama watangulizi wake katika afisi hii, Mbadi alionekana mwingi wa bashasha, akiongoza bajeti ya kitaifa ya mwaka wa 2025/2026. Na kama ilivyo mazoea, waziri Mbadi alifanya kama wenzake, kutembea na mkoba wenye karatasi zenye mapendekezo ya makadirio ya bajeti.