Shughuli ya kuwasajili wakaazi wa kaunti ya Samburu katika bima ya afya ya SHA inaendelea

  • | K24 Video
    102 views

    Shughuli ya kuwasajili wakaazi wa kaunti ya Samburu katika bima ya afya ya SHA inaendelea, lakini unakumbwa na changamoto kubwa katika kufanikisha upokeaji mpana wa mpango huo. Kufikia mwishoni mwa mwaka 2024, ni takriban asilimia 5 tu ya wakazi wa kaunti ya Samburu, waliokuwa wamejisajili kwa mpango wa bima ya afya ya jamii (SHA), jambo linaloifanya kuwa miongoni mwa kaunti zenye viwango vya chini zaidi vya usajili wa kitaifa.