Ni kwa nini Tundu Lissu ameamua kujitetea mwenyewe mahakamani?

  • | BBC Swahili
    48,219 views
    Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania, na mwenyekiti wa chama cha upinzani CHADEMA Tundu Lissu ameomba rasmi kuwaondoa mawakili wake na kuamua kujitetea mwenyewe katika kesi ya uhaini inayomkabili. Uamuzi huu unamaanisha kuwa atakuwa akishiriki moja kwa moja katika mabishano ya kisheria na mawakili wa serikali bila uwakilishi wa mawakili wake wa awali.