Wanawake kaunti ya Pokot magharibi ambao ni manusura wa ukeketaji wafuzu mafunzo ya ujasiriamali

  • | K24 Video
    38 views

    Zaidi ya wanawake 700 katika kaunti ya Pokot magharibi ambao ni manusura wa ukeketaji na ndoa za mapema, wamefuzu mafunzo ya ujasiriamali, na mafunzo ya kiufundi. Mpango huu unawapa hifadhi salama, mafunzo ya kiufundi kuwasaidia kuanza maisha mapya, pamoja na kuwawezesha kifedha, kwa kuonyesha mshikamano na kuunga mkono juhudi hizo, viongozi mbalimbali wakiwemo wajasiriamali na wadau wengine, wametoa wito kwa serikali kuendeleza miradi sawia, ili kuleta mabadiliko endelevu yanayoongozwa na wanawake, kuwanusuru wanawake.