NCIC yahamasisha wanafunzi kuhusu umuhimu wa Amani

  • | Citizen TV
    161 views

    Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano, NCIC imezidisha juhudi za kukuza amani shuleni kwa kutumia vilabu vya amani kama njia ya kuzuia utumizi wa mihadarati, ghasia, na uhalifu miongoni mwa wanafunzi, hasa katika maeneo ya Pwani Akizungumza katika shule ya upili ya Kwale High, Afisa Mkuu Mtendaji wa NCIC, Daniel Mutegi, amesema kuwa vilabu hivyo vimekuwa chombo muhimu katika kusuluhisha mizozo kati ya shule mbalimbali na pia baina ya walimu na wanafunzi. Alieleza kuwa vilabu hivyo vinalenga kuwalea wanafunzi kuwa mabalozi wa amani ndani na nje ya shule.