Wananchi wapewa huduma za Afya kaunti ya Kajiado

  • | Citizen TV
    49 views

    Shirika la Amref kwa ushirikiano na Wizara ya Afya katika kaunti ya Kajiado limeanza kutekeleza mpango wa one health, ambao unajumuisha wakazi kupewa matibabu ya bure pamoja na kutoa chanjo kwa mifugo na wanyama wengine wa nyumbani kama vile mbwa na paka. Mpango huo ambao unatarajiwa kudumu kwa kipindi cha miaka mitano unalenga kuhakikisha kuwa magonjwa ya kuambukuza kutoka kwa wanyama hadi kwa binadamu yanakabiliwa na hivyo kupunguza mzigo wa mtibabu kwa umma.