Washukiwa 19 wa vurugu za Ol Kalou waachiliwa

  • | Citizen TV
    1,032 views

    Watu 19 waliohusishwa na vurugu la Gen Z eneo la Olkalou kaunti ya Nyandarua wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja kila mmoja. Hakimu wa Nyandarua Judicaster Nthuku alisema kuwa hakuna sababu ya kuendelea kuwazuilia washukiwa hao kwa siku 21 kama ulivyotaka upande wa mashtaka. Haya yanajiri huku mshukiwa mmoja akizuiliwa Kiambu kwa kupatikana na vifaa vilivyoibwa wakati wa maandamano hayo.