Helikopta ya kijeshi ya Uganda yaanguka Mogadishu

  • | BBC Swahili
    1,510 views
    Helikopta ya kijeshi imeanguka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aden Adde mjini Mogadishu Jumatano asubuhi. Picha zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha moshi mzito ukipanda kutoka uwanja wa ndege, unaoripotiwa kusababishwa na moto uliozuka kufuatia ajali hiyo. Watu wanane walikuwa ndani ya ndege hiyo, wakiwemo marubani. Hatima ya waliokuwemo bado haijulikani kwa sasa. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika, lakini uchunguzi unaendelea. #bbcswahili #somalia #mogdishu Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw