Mbunge kenya apendekeza mswada wa udhibiti wa mikusanyiko

  • | BBC Swahili
    3,722 views
    Jumatatu ya Julai saba mwaka huu , vijana wa rika wa Gen Z nchini Kenya wamepanga tena kuendeleza maandamano yao ya kuishinikiza serikali ya sasa kuheshimu katiba kwa kutowezesha mauaji, utekaji nyara na kukamatwa kwa wanaopinga sera za serikali ya rais William Ruto. - Huku vijana wakijiandaa kwa kile wanadai ni maandamano makubwa kuliko yaliyoshuhudiwa Juni 25 katika maadhimisho ya mwaka mmoja tangu yale ya 2024 ambapo Bunge lilivamiwa, serikali inaweka mikakati ya kudhibiti maandamano hayo kwa kupendekeza kufanyiwa mabadiliko katika sheria ya kusimamia ukusanyikaji wa watu. - Akiwasilisha pendeekzo hilo, rais William Ruto alitaja kwamba maafa yanayotokea kwenye maandamano hayo na vile vile hasara wanayopata wafanyabiashara wadogo na hata majengo ya kiserikali ni hali ambayo kamwe haitokubaliwa kuendelea kutokea. - @RoncliffeOdit anachambua kwa kina suala hili na mengine mengi katika Dira ya Dunia TV kwenye ukurasa wa YouTube BBC Swahili. - - - #bbcswahili #kenya #maandamano Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw