Familia ya Albert Ojwang' inazidi kulilia haki

  • | Citizen TV
    1,832 views

    Familia ya Mwanablogu aliyeuawa seli ya polisi jijini Nairobi Albert Ojwang' imeendelea kudai haki kutoka kwa serikali kuhusu mauaji yake, ikitaka majibu ya lengo kuu haswa la kukamatwa kwake na kisha kuuawa. Kwenye ibada ya mazishi iliyoandaliwa katika kanisa la Ridgeways Baptist, hapa Nairobi, familia ya Ojwang' imesema haitapumzika hadi haki itakapopatikana