Diddy akutwa na hatia ya mashtaka mawili

  • | BBC Swahili
    3,693 views
    Sean "Diddy" Combs amekutwa hana hatia ya uhalifu wa kupanga (racketeering), na pia hana hatia ya usafirishaji haramu wa ngono dhidi ya aliyekuwa mpenzi wake Casandra Ventura na mwanamke mwingine anayetambulika kama "Jane". Hata hivyo, alipatikana na hatia ya usafirishaji kwa ajili ya kujihusisha na ukahaba, kuhusiana na wanawake wote wawili. kila kosa alilopatikana na hatia linabeba kifungo cha hadi miaka 10, hivyo anaweza kukabiliwa na jumla ya hadi miaka 20 gerezani. Combs, mwenye umri wa miaka 55, amekanusha mashtaka yote.- #bbcswahili #newyork #marekani Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw