- 254 viewsDuration: 1:11Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe, amewataka viongozi wa kisiasa kukoma kutumia bei ya majani chai kama silaha ya kisiasa akisema changamoto zilizopo katika sekta ya majani chai ni za kiufundi na zinahitaji suluhu za sera na kuboresha ubora wa mazao. Kagwe amesisitiza kuwa wakulima wako huru kuuza chai popote wanapopata bei nzuri akiwaonya viongozi dhidi ya kuigawa sekta hiyo kwa misingi ya kikanda.