Polisi wakanusha madai kwamba wahuni walivamia eneo la Ruiru

  • | KBC Video
    371 views

    Maafisa wa polisi wamekanusha madai kuhusu uporaji uliotekelezwa jana na wahuni mjini Ruiru katika kaunti ya Kiambu. Kulingana na wakazi wahuni hao waliwahangaisha huku wakivunja biashara zao. Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Ruiru Charles Kibathi amepuuzilia mbali madai hayo akisema ni uvumi usio na msingi akiwahakikishia wakazi kwamba hakukuwa na tukio kama hilo. Wakati huo huo maafisa wa polisi wamesema wataimarisha uchunguzi kwa saa 24 katika eneo hilo ili kurejesha utulivu kufuatia maandamano ya hivi maajuzi ya Sabasaba yaliyozua ghasia ambapo biashara kadhaa ziliporwa na mali kuharibiwa.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive