Ruto atoa onyo kwa wanaoharibu mali ya umma. Katika Dira ya Dunia TV

  • | BBC Swahili
    10,025 views
    Rais wa Kenya William Ruto amevunja kimya chake kuhusiana na ghasia zilizoshuhudiwa katika majimbo 17 Jumatatu ya Julai saba ambapo watu 31 waliuawa katika makabiliano kati ya makundi ya vijana na polisi. Katika hotuba yake mapema leo, Ruto ametangaza vita vikali dhidi ya wenye kupanga na kutekeleza ghasia hizo akiapa kwamba kamwe hatokubali tena uharibifu wa mali ya wafanyabiashara na wahuni waliolipwa kusababisha ghasia.