Watu watano waliuawa kwa risasi maandamano wengine 40 bado watibiwa KNH

  • | Citizen TV
    874 views

    Upasuaji wa maiti ya waathiriwa watano wa maandamano ya saba saba umeonyesha kwamba walifariki kwa majeraha ya risasi. Aidha, risasi mbili zimepatikana kwenye miili ya waathiriwa wawili Paul Makori na Anthony Maina waliopigwa risasi na maafisa wa polisi eneo la Kangemi na Kahawa West siku ya maandamano ya Saba Saba. Watu arobaini wakiwemo watoto wanapokea matibabu katika hospitali kuu ya Kenyatta wakiwa na majeraha ya risasi