Naibu Gavana wa Kaunti ya Kericho,Fred Kirui ataka uchunguzi wa malipo hewa

  • | Citizen TV
    148 views

    Naibu Gavana wa Kaunti ya Kericho,Fred Kirui, ametaka uchunguzi wa haraka kufanywa kuhusu madai ya malipo hewa ya takriban shilingi milioni 80 yaliyolipwa kwa wakandarasi na wasambazaji bidhaa. Kirui, ambaye kwa muda sasa amekuwa na mvutano na Gavana Erick Mutai alidai kuwa fedha hizo zililipwa kwa kampuni zisizopungua 33 kwa bidhaa ambazo aidha hazikusambazwa au hazikununuliwa kwa kufuata taratibu za uagozaji bidhaa. ‎Kwa mujibu wa Kirui, malipo hayo yalifanyika kati ya mwezi wa Oktoba 2024 na Aprili 2025