Israel yazidi kuishambulia Gaza. Katika Dira ya Dunia TV

  • | BBC Swahili
    7,661 views
    Watu 139 wameuawa huko Gaza katika muda wa saa 24 zilizopita kufuatia mashambulizi ya anga. Kwa mujibu wa maafisa wa huduma za dharura, watoto sita walikuwa miongoni mwa watu kumi waliouawa walipokuwa wakisubiri kujaziwa maji kwenye vyombo vyao, katika kambi ya wakimbizi ya al -Nuseirat katikati mwa Gaza Israel imelaumu shambulizi hilo kwa kile ikichokiita hitilafu ya kiteknolojia ambapo shambulizi lilitekelezwa mita chache kutoka kwa gaidi aliyekuwa akilengwa.