Wakenya washauriwa kujiunga na mashirika ya kijamii ili kujiendeleza

  • | Citizen TV
    400 views

    Wakenya kutoka matabaka tofauti wameshauriwa kujiunga na mashirika ya kijamii kama njia mojawapo ya kukabili ugumu wa maisha hususan nyakati za majanga. Wakizungumza mjini Kisii , wadau kutoka mashirika mbalimbali wamewarai wakenya kuiga umoja wa shirika moja mjini Kisii ambalo limezua gumzo kwa kuzindua mradi wa gari maalum la biashara linalomilikiwa na wanachama hao. Wito umetolewa kwa wajane, vijana na wasiojiweza katika jamii kuungana na mashirika kama hayo ili kuepuka msongo wa mawazo wakati janga linapobisha hodi..