Hospitali 120 zimefungwa na serikali huko Kisii

  • | Citizen TV
    532 views

    Wizara ya afya kupitia bodi ya KMPDC imeamrisha kufungwa mara moja kwa hospitali 120 katika kaunti ya Kisii. Hii ni kutokana na ukaguzi uliofichua kuwa hospitali hizo hazikuwa zimefikia viwango vilivyowekwa. Hayo yanajiri wiki chache baada ya oparesheni sawia kufanyika katika kaunti nyingine tano ambapo zaidi ya hospitali 800 zimeamrisha kusitisha kutoa huduma kwa wananchi.