UN yalaani mauaji ya zaidi ya watu 40 DRC

  • | BBC Swahili
    1,803 views
    Ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO) umelaani vikali shambulio huko Komanda, takriban kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, mji mkuu wa Ituri", lililowauwa takriban watu 43 wakiwemo wanawake na watoto. Umoja wa Mataifa na Jeshi la Congo walisema kwamba raia waliohudhuria ibada ya mkesha katika kanisa la eneo hilo walikatwa kwa mapanga, na kusababisha vifo vya watu hao. Je hatua hii inamaanisha nini kwa usalama mashariki mwa DRC? Jiunge na Martha Saranga saa tatu usiku katika Dira ya Dunia TV. Na pia usisahau kutembelea ukurasa wetu wa youtube wa bbcswahili ambapo unatupata mubashara. #bbcswahili #DRC #congo Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw