Katibu wa Usalama Raymond Omollo ataka Wakenya kujivunia kuandaa dimba la CHAN

  • | Citizen TV
    217 views

    Zikiwa zimesalia chini ya saa 24 kabla ya kuanza kwa mechi kati ya Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, katibu wa usalama wa kitaifa Raymond Omollo amewataka wakenya kujivunia kuandaa dimba la chan kwani ni mara ya kwanza tangu mwaka 1987 ambapo taifa linaanda mchuano wa aina hii. Dkt. Omollo anasema mipangilio yote imekamilika kabla ya mechi hiyo itakayochezwa uwanjani Kasarani.