Foleni zashuhudiwa kufuatia uhamisho wa mfumo wa SHA kwenda dijitali

  • | Citizen TV
    1,057 views

    Mkanganyiko na foleni ndefu za wagonjwa zimeshuhudiwa kwenye hospitali kadhaa nchini, katika shughuli ya kuhamisha mfumo wa SHA kwa njia ya dijitali. Kutoka hospitali za Kisii hadi Nakuru, waliofika kupata huduma walihangaika kuhamishwa kwa maelezo yao kwenye mfumo wa dijitali. Hata hivyo, baadhi ya hospitali zilifanya uhamisho huu bila tabu zozote, siku moja baada ya wizara ya afya kupiga marufuku utumizi wa uthibitisho wa OTP kwa wanaotibiwa kupitia SHA