Spika Job Ndugai atakumbukwa kwa lipi?

  • | BBC Swahili
    9,007 views
    Aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Yustino Ndugai amefariki dunia hapo jana jioni. Taarifa zinasema Ndugai aliugua ghafla na alifariki akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali moja jijini Dodoma. Ndugai aliyefariki akiwa na umri wa miaka 62 amehudumu kwanza kama Naibu Spika kwa miaka mitano kati ya mwaka 2010 hadi 2015 na baadae kuwa Spika kamili kwa miaka saba, tangu mwaka 2015 hadi mwaka 2022. - Katika Makala hii, Sammy Awami anaangazia mambo machache tu ambayo Spika Ndugai atakumbukwa kwayo…