Gachagua amjibu Kindiki, akataa kuhojiwa na polisi

  • | Citizen TV
    9,706 views

    Kinara wa DCP Rigathi Gachagua amepuuzilia mbali matamshi ya naibu rais Kithure Kindiki na waziri wa usalama kipchumba murkomen kuwa anapaswa kuandikisha taarifa na idara ya upelelezi kwa matamshi yake ya punde kuhusu ugaidi. Akizungumza kwenye ziara yake ya marekani, Gachagua amesema yuko tayari kutoa habari muhimu kwa marekani kuhusiana na madai yake kuhusu ushirikiano wa rais william ruto na kundi la waasi la Sudan kusini la rsf. Hata hivyo, ameshikilia kuwa hataandikisha taarifa na polisi wa kenya.