Murkomen amwamuru Gachagua kutoa taarifa kwa DCI kuhusu madai ya uhusiano wa Serikali na Magaidi

  • | Citizen TV
    3,621 views

    Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen sasa anasema ni lazima kwa kinara wa DCP Rigathi Gachagua aandikishe taarifa na Idara ya upelelezi kuhusiana na madai kwamba serikali ya kenya ina uhusiano na makundi ya kigaidi, pindi atakaporejea nchini. Murkomen akisisitiza kuwa serikali haitomruhusu Gachagua kuendelea kuipaka serikali tope ughaibuni kwa kile alichokitaka kuwa propaganda isiyo na msingi