Mwanamke bomba | Priscillah Nyairia, mvumbuzi wa Kilimo cha Matunda Laikipia

  • | Citizen TV
    363 views

    Priscilla Nyairia amepata umaarufu kwa ujuzi wake na ubunifu katika kilimo. Priscilla anajihusisha na kilimo na kutoa mafunzo kwa wakulima wa matunda. Kwenye makala ya Mwanamke Bomba juma hili, tunamuangazia priscillah, mwanamke mwenye umri wa miaka 25 ambaye amezidisha kilimo cha matunda kutoka kwenye ardhi ya ekari mbili hadi ekari Hamsini katika kipindi cha miaka mitano. Priscilla pia ameajiri vijana zaidi ya mia tatu katika eneo la makutano, kaunti ya Laikipia