Tazama kanisa zima laanza safari ya siku mbili kuvuka jiji la Uswidi.

  • | BBC Swahili
    4,767 views
    Kanisa la kihistoria lenye umri wa miaka 113 ambalo liko hatarini kuporomoka limehamishwa lote kwa pamoja umbali wa kilomita 5 (maili 3) barabarani kaskazini mwa Sweden. Kwa mwendo wa mita 500 kwa saa, safari hiyo imechukua siku mbili (Agosti 19–20). Mji huo wa zamani katikati ya jiji upo hatarini kutokana na mipasuko chini ya ardhi baada ya zaidi ya karne moja ya uchimbaji wa madini ya chuma. Kampuni ya uchimbaji wa madini ya chuma, LKAB ndio inalipia gharama ya uhamishaji wa jiji hilo, inayokadiriwa kufikia zaidi ya bilioni moja. #bbcswahili #sweeden #kanisa Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw