Wafuasi wa Gachagua wakabiliwa na wahuni JKIA | Watu wajeruhiwa

  • | Citizen TV
    9,377 views

    Kurejea kwa kinara wa DCP Rigathi Gachagua nchini kulikumbwa na vurugu na vurumai baada ya wahuni kukabiliana na wafuasi wa Gachagua wakati msafara wake ulipokuwa ukitoka uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta. Vijana hao waliojihami na silaha na mawe waliwarushia viongozi walioandamana na Gachagua huku magari yakiharibiwa na hata watu kadhaa wakijeruhiwa