CHAN yafanikisha kuongeza idadi ya mashabiki watakaotazama mechi ya Harambee stars Kasarani

  • | Citizen TV
    291 views

    Imekuwa afueni kwa wapenzi wa kandanda nchini baada ya serikali kutangaza kuwa shirikisho la kandanda barani Afrika limekubali kuongeza idadi ya mashabiki watakaotazama mechi moja moja katika uwanja wa Kasarani. Waziri wa Michezo Salim Mvurya sasa akisema mashabiki elfu 36 sasa wataweza kufuatia mechi ya robo fainali kati ya Harambee Stars, na Madagascar hapo kesho. Idadi hii ikiongezeka kutoka mashabiki elfu 27