Mwanamke Bomba - Mafanikio ya Jamila Kizondo katika kueneza lugha ya Kiswahili mtandaoni

  • | Citizen TV
    359 views

    Wengi waliotangamana naye wanamfahamu kwa kuenzi lugha ya Kiswahili na hata kuzungumza lugha hii kwa ustadi hadi nchini Marekani. Jamila Kizondo si mgeni kwa wanaotumia mitandao ya Kijamii, akianza umaarufu wake mtandaoni kwa kutoa mafunzo kuhusu lugha ya Kiswahili na Uswahili. Kutoka kwa mizizi yake maeneo ya Pwani, Jamila Kizondo sasa amekuwa balozi wa Lugha ya Kiswahili si tu nchini Marekani, bali hata uarabuni