- 30,712 viewsDuration: 3:01Maridhiano baada ya maandamano na ghasia za siku ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, ndiyo mada inayotawala mijadala nchini Tanzania kwa sasa. Jumuiya ya Madola imemteua aliyekuwa rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, kuongoza juhudi hizi za kuleta maridhiano. Hatua hiyo imepokewa kwa maoni tofauti kutoka kwa makundi mbalimbali, yakiwemo wanasiasa, taasisi za kiraia, na viongozi wa madhehebu tofauti ya dini. Mwandishi wa BBC @kaijageflo1 anatueleza zaidi - - #bbcswahili #tanzania #siasa #uchaguzi2025 #Maandamano