Uteuzi wa mgombea mwenza wa muungano wa Azimio

  • | K24 Video
    74 views

    "Martha Wangari Karua ndiye chaguo bora la mgombea mwenza wa muungano wa Azimio" si maneno yangu bali ni tangazo rasmi lililotolewa hii leo na kinara wa ODM Raila Odinga baada ya jina la Karua kupendekezwa na jopo lililopewa jukumu la kuwahoji walioonyesha ari ya kuwa mgombea mwenza wa muungano wa Azimio. Ugavi wa mamlaka pia umesheheni leo katika ukumbi wa KICC, Odinga akiahidi vyeo kwa baadhi ya wandani wake wa kisiasa endapo muungano wa Azimio utafanikiwa kuunda serikali ijayo.