- 242 viewsDuration: 8:04Huku watu wenye ulemavu humu nchini wakijiunga na ulimwengu kuadhimisha siku ya watu wenye ulemavu duniani, kundi moja la walemavu katika kaunti ya Kajiado limeandaa matembezi ya kuhamasisha Jamii kuhusu haja ya kuwajumiisha katika miradi mbalimbali pamoja na uongozi . Kwenye matembezi hayo ambayo yanaandaliwa Mjini Kajiado watu wenye ulemavu wanataka Haki zao zizingatiwe zikiwemo Usalama, Elimu Bora na Mazingira mazuri ya kufanyia kazi zao za kila siku