- 3,463 viewsDuration: 5:40Wanyama kama nyani kwa Kawaida wanaishi vizuri kwa misitu, lakini katika soko la Wamba Kaunti ya Samburu, nyani hawa wanaishi sokoni. Wakaazi wanasema nyani hao huokota chakula kwenye maeneo ya kutupa taka na wakati mwingine wanaingia ndani ya nyumba za watu kutafuta chakula. Wengi wanaamini kuongezeka kwa nyani katika soko hili kumetokana na ukosefu wa chakula na kuharibiwa kwa misitu kama anavyoarifu Susan Ndunda.