- 334 viewsWaziri wa madini na uchumi wa baharini na maziwa Ali Hassan Joho amesema kuwa wizara hiyo itahusisha umma katika mazungumzo ya kutatua mzozo ulioibuka kuhusu mpango wa kuchimba madini ya dhahabu eneo la Ikolomani kaunti ya Kakamega.akiongea baada ya kutia saini mkataba wa makubaliano na serikali ya kaunti ya Kakamega, Joho alisema kuwa maslahi ya wenyeji yatapewa kipaumbele hasa katika suala la fidia.