Wataalamu wa afya wamezua hofu juu ya ongezeko la magonjwa yanayohusiana na mitindo ya maisha kama vile kisukari, shinikizo la damu na aina mbalimbali za saratani ambazo zimeathiri familia kote nchini. Hofu hiyo iliibuliwa wakati wa kambi ya matibabu ya bila malipo huko Gachororo, eneo bunge la Juja kaunti ya Kiambu, ambako wataalam wa afya walifichua kuwa wakazi wengi wanapambana kimyakimya na magonjwa sugu kutokana na huduma duni za afya na gharama ya juu ya huduma za matibabu.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive