Mamia ya wazee waonya wanaovuruga usalama Samburu

  • | Citizen TV
    1,117 views

    Wazee wa Jamii ya Wasamburu wameonya wanaohusika kwenye uhalifu kuwa watakabiliwa vikali kisheria. Mamia ya wazee waliokutana eneo la Ndikirr Olngwesi, Samburu ya kati waliwaonya wahalifu haswa wanaotekeleza wizi wa mifugo. Visa vya uhalifu zimeripotiwa kuongezeka katika maeneo mengi kaunti ya Samburu, hali iliyowaacha wakazi kuishi kwa hofu. Wazee hawa wameilaumu serikali kwa kulegeza kamba, huku chifu wa Lulu Christine Leleshep akiahidi ushirikiano kuhakikisha usalama maeneo hayo