- 12,155 viewsDuration: 3:19Kiwango cha umaarufu na uungwaji mkono wa chama cha ODM kinaonekana kupungua kutoka asilimia 38 mwezi Septemba mwaka uliopita hadi asilimia 19 mwezi huu. Kwenye kura ya hivi punde zaidi ya maoni iliyotekelezwa na kampuni ya Infotrak, baina ya tarehe 19 na 20 mwezi huu kiwango cha umaarufu cha chama tawala cha UDA kimeongezeka hadi asilimia 23 kutoka asilimia 16 mwezi Agosti mwaka huu. Kura hiyo pia ilibainisha kuwa rais William Ruto ndiye mgombea maarufu zaidi wa urais iwapo uchaguzi ungeandaliwa leo kwa asilimia 28 akifuatiwa na Fred Matiang’i kwa asilimia 13 naye Kalonzo Musyoka akiwa wa tatu kwa asilimia 12. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive