Indonesia: Mkanyangano wa watu katika uwanja wa soka uliosababisha vifo vingi

  • | BBC Swahili
    632 views
    Baba wa wasichana wawili waliouawa katika mkanyagano katika uwanja wa mpira wa miguu nchini Indonesia ameita maafa hayo "mauaji, si ghasia za soka". Mke wa zamani wa Devi Athok pia alikufa pamoja na binti zao kwenye mkanyagano wa Jumamosi. Takriban watu 131 waliuawa wakati maelfu ya mashabiki walipokimbilia uwanjani baada ya timu ya nyumbani kupoteza mchezo kwenye uwanja wa Kanjuruhan huko Malang, Java Mashariki. Polisi walijibu kwa kurusha mabomu ya machozi. Mkuu wa jeshi la polisi mkoani humo ameomba radhi kwa kasoro za namna ulinzi ulivyosimamiwa uwanjani hapo. Uchunguzi wa jinai kuhusu tukio hilo sasa unaendelea. #bbcswahili #indonesia #michezo